Breaking

Tuesday 1 November 2022

WASHINDI MR & MISS DEAF WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO



Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imetekeleza ahadi ya (Royal Tour) kuwapeleka washindi wote wa Shindano la Dunia la Urembo Utanashati na Mitindo kwa viziwi na viongozi kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii kwenye Hifadhi ya Ngorongoro Mkoa Arusha.

Washindi wa shindano hao wameanza ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro leo Novemba 1, 2022.

Mhe. Mchengerwa amesema tayari washindi wapo katika siku ya kwanza ya ziara ya kwa gharama za Serikali.

Amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kutumia michezo, Sanaa na utamaduni kuitangaza Tanzania duniani na kuinua uchumi wake.

Tunatarajia washindi hawa watafurahia vivutio mbalimbali vilivyopo kwenye Hifadhi ya Ngorongoro na watakuwa mabalozi wazuri watakaporejea katika nchi zao.


Katika shindano hilo, mtanzania Hadija Kanyama ametwaa taji la Dunia la Urembo, wakati kwa upande wa Utanashati mtanzania Rajan Ally ameibuka mshindi wa pili na mtanzania mwingine Russo Songoro ameshinda taji la wanaume utande wa Mitindo.




Tanzania imekuwa nchi ya kwanza katika Bara la Afrika na ya 12 duniani kuandaa na kuwa mwenyeji wa shindano hilo.
Mtendaji Mkuu wa Shindano hilo Bonita Annleek amefafanua kwamba shindano la mwaka huu limefanyika kwa mafanikio makubwa huku akisisitiza kwamba Tanzania ilipewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa shindano hilo kutokana na rekodi ya Amani na vivutio vya utalii, ukarimu na Ushirikiano wa nchi nyingine.







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages