Breaking

Sunday 27 November 2022

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI




Na Richard Mrusha

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao itakayosaidia kupunguza tatizo la rushwa inayosababishwa na wananchi kukutana na watendaji mara kwa mara katika kupatiwa huduma.

Waziri Mhagama ameyasema hayo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya kwanza ya mamlaka ya serikali mtandaoni

Ameelekeza Bodi hiyo kusimamia vizuri majukumu yao ili kuondosha tatizo la rushwa kwasabu ya wananchi kukutana na watendaji mara kwa mara na kurahisha upatikanaji wa rushwa.

amesema juhudi zinazofanywa na Serikali ni kuhakikisha huduma zinafanyika kidigitali na kuchangia ukusanywaji mzuri mapato na kupelekea kuongezeka.

amesema Mamlaka hiyo imebeba siri kubwa ya matumizi ya mtandao na nia ya serikali ni kuajiri watu waaminifu na wazarendo watakaosimamia mifumo ya tehama.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya serikali mtandao,Mhandisi Benedict Benny amesema mamlaka hiyo utekelezaji wake watasimamia jitihada za serikali mtandao katika ujenzi wa mifumo shirikishi na ya kisekta.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya wakuregenzi,Dkt Mussa Muhiddin,amesema watafanya kazi kwa ushirikiano kwa kufuata kanuni za za serikali mtandao.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages