Breaking

Tuesday 27 December 2022

AJIUA KWA SUMU KISA PESA YA SODA



Bukindu Mhoja (22), mkazi wa Kitongoji cha Bugogo, Kata ya Bukoli mkoani Geita amejiua kwa kunywa sumu, baada ya kudaiwa hajalipa shilingi 45,000 ya soda alizokuwa ameagizwa kwenye duka la Masikio ambaye alimpokonya vinywaji na kumsema kwa maneno mabaya.

Hali iliyopelekea wazazi kugoma kuzika mwili wa mtoto wao mpaka watakapojua hatma ya waliosababisha mtoto wao kujiua.

Kaka wa marehemu Yohana Emmanuel anaelezea sababu za wao kugomeea kuuzika mwili wa marehemu huku mama mzazi wa Marehemu Shija Antony anaelezea jinsi mwanae alivyofika nyumbani akajifungia ndani na kunywa sumu.

"Tutachukuaje mwili wa marehemu hamjawachukua maelezo sehemu zote mbili, hatujaona yule aliyemtuma kwamba mmemchukua maelezo alafu na kule alikokuwa ametumwa mmechukua maelezo, nimawaambia mapolisi kwamba sisi hatuwezi tukachukua mwili wa Marehemu na hata kama tukiuchukua inatakiwa tuupeleke kule alipokuwa ametumwa kwenye soda ", alisema Emmanuel.

"Ametoka mule ndani na kikombe cha maji akaingia kwake akafunga alivyofunga hivyo nikamsikia anatapika, nikamwambia wewe umefanyaje nikausukuma mlango alikuwa ameurudisha tu, umefanyaje, amenyamaza tu anatapika tu, baadaye katoka nje akawa anatembeatembea tena akaingia ndani akachukua kikombe cha maji akanywa alipomaliza kile kikombe kunywa akarudi ndani akalala akanambia mama, nilipotoka hapa ilifika nikatumwa na Roba soda kwa Masikio nimefika kule nikampa mke wa Masikio zile hela akanipa soda kwa baadae tena nimetembea hatua mbili akasema hujanilipa hela rudisha hizo soda ndio maana mama nimeamua ninywe sumu sababu na zamani nilimfanyia kazi penyewe siku mbili akanidhurumu", Alisema Mama wa kijana huyo.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Ally Kitumbu, amekiri kutokea kwa tukio hilo ambalo bado wanalifanyia uchunguzi, "Hiyo taarifa ya mtoto kunywa sumu tunayo lakini bado tunaichunguza nafikiri ikiwa tayari tutaizungumzia vizuri, niiombe jamii ya mkoa wa Geita na maeneo mengine kwamba kuna mambo amabyo yakikupata unaweza ukatafuta njia sahihi ya kuyatatua badala ya kujiua,".

Via: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages