Breaking

Tuesday 13 December 2022

MFUKO WA SANAA WAPATA VIFAA, DKT. ABBAS AONGOZA MAANDALIZI TUZO ZA MUZIKI 2022



Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi leo Desemba 13, 2022 amekagua na kukabidhi vifaa vya kisasa vitakavyotumiwa na Ofisi ya Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa.

Dkt. Abbasi amekabidhi vifaa hivyo kwa Mratibu wa Mfuko huo Mfaume Said ikiwa ni juhudi za Wizara hiyo chini ya Waziri Mohamed Mchengerwa, kuuwezesha Mfuko kuanza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi katika sekta hizo.



Mfuko huo umetengewa kiasi cha shilingi Bilioni 3.9 kwa Mwaka wa Fedha 2021 hadi 2023 na vifaa hivyo vitakapofika vyote vitagharimu TZS milioni 90.

Katika hatua nyingine, Dkt. Abbasi ameongoza kikao cha Bodi ya Baraza la Sanaa nchini (Basata), ambapo miongoni mwa nyaraka zilizojadiliwa ni Mwongozo wa Maadili kwa Wasanii na Mwongozo wa Maandalizi ya Tuzo za Muziki (TMA) za mwaka 2022 lakini zitatolewa April, 2023.




Ametumia fursa hiyo kuwaagiza watendaji kadhaa wapya waliohamishiwa Basata kutoka taasisi mbalimbali za umma ikiwa ni sehemu ya maboresho na wale wa zamani kuendeleza umoja na ubunifu kwani sekta ya sanaa ni moja ya sekta za kimkakati kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages