Breaking

Wednesday 14 December 2022

RAIS DKT. MWINYI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi arnefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:

I. Tume ya Mipango:

(i) Dkt. Ameir Haji Sheha ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara ya Ukuzaji Uchumi. Dkt. Ameir aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

(ii) Ndugu Mohamed Masoud Salim ameteuliwa kuwa Kamishna wa

Idara ya Mipango ya Kitaifa, Maendeleo ya Kisekta na Kupunguza Umaskini. Kabia ya uteuzi Ndugu Mohamed alikuwa Meneja wa Pensheni katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

(iii) Dkt. Rukkaya Wakif Muhammed ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara ya Mipango na Maendeleo ya Watendakazi. Kabla ya uteuzi Dkt. Rukkaya alikuwa Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU).

2. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ:

Ndugu Zainab Khamis Kibwana ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kabla ya uteuzi Ndugu Zainab a.likuwa Mwanasheria katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

3. Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi:

Ndugu Zahor Salum Elkharous ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uratibu wa Uchumi wa Buluu Zanzibar. Ndugu Zahor aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu Tanzania.

4. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto:

Ndugu Bihindi Nassor Khatib ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti. Ndugu Bihindi aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZURA.

(ii) Ndugu Sitti Abass Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Jamii. Kabla ya uteuzi Ndugu Sitti alikuwa Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa, Maendeleo ya Kisekta na Kupunguza Umasikini

(iii) Ndugu Hassan Ibrahim Suleiman ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee. Kabla ya uteuzi Ndugu Hassan alikuwa Mwalimu katika Skuli ya Sekondari ya Haile Salassie.

Uteuzi huo unaanzia Ieo tarehe 14 Disemba, 2022.

(Mhandisi Zena A. said)

KATIBU WA BARAZA LA MAPINDUZI NA KATIBU MKUU KIONGOZI, ZANZIBAR.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages