Breaking

Sunday 25 December 2022

"WATANZANIA OMBENI MSAMAHA KWA MUNGU" DKT. MPANGO



(Picha na OMR).

NA MWANDISHI WETU


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango ametoa wito kwa Watanzania kuomba toba kwa Mungu kwa matendo ya kikatili hususani kwa watoto na kuacha dhuluma dhidi yao, huku akiwasihi kutimiza mahitaji ya watoto katika kuwatunza ikiwemo kuhakikisha wanapata elimu.

Akizungumza leo Desemba 25, 2025 baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Krismasi katika Parokia ya Kristo Mfalme, Veyula mkoani Dodoma, Makamu wa Rais pia ametoa wito kwa Watanzania kuongeza jitihada katika kuimarisha ulinzi wa watoto ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyowakumba.

Kuhusu mvua zilizoanza kunyesha hapa nchini, Makamu wa Rais pia ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya uwepo wa mvua hizo katika kuzalisha mazao na kupanda miti ili kuhifadhi mazingira.



Amesema, ni muhimu suala la upandaji miti kuanza katika ngazi ya familia kwa kupanda miti mitatu kila familia na hivyo kupendezesha nchi na kulinda mazingira.

Katika ibada hiyo, Makamu wa Rais ameambatana na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango na ibada imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme iliyopo Veyula Dodoma Padre Saimon Katembo
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages