Breaking

Tuesday 31 January 2023

MWALIMU MSTAAFU MAHAKAMANI KWA KUTOA RUSHWA



Na Lucas Raphael,Tabora

TAASISIS ya kuzuia na kupambana na Rushwa wilaya ya Igunga mkoani Tabora imefikisha mahakamani mwalimu mstahafu aliyekuwa anafundisha shule ya msingi Mwanzugi kwa tuhuma ya kutoa rushwa ya shilingi 500,000 kwa afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga .

Mwendesha mashitaka wa Takukuru wilaya ya Igunga Mizengo Joseph jana aliambia mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Edda Kahindi kwamba mnamo juni 24 mwaka 2022 majira ya saa tano asubuhi katika ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Igunga mshitakiwa Jesca Jones Yegela alimshawishi afisa Utumishi Erick Size ampe shilingi 500,000/ ili aweze kumsaidia kwenye madai yake ya mapunjo ya mshahara baada ya kustahafu.



Alisema kwamba mshitakiwa anakabiliwa na mashitaka mawili ya kumshawishi na kutoa rushwa ya shilingi 300,000/ ili kumsaidia kwenye mapunjo ya mshahara baada ya kustaafu.

Mizengo aliendelea kuiambia mahakama hiyo kwamba mshitakiwa alitenda makosa hayo kinyume na kifungu namba 15 (i)b na (2 )cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa ,sura namba 329 mapitio ya mwaka 2019.

Hata hivyo mshitakiwa huyo alikama tuhuma hizo na sasa yupo nje kwa dhamana ya shilingi 500000/ na kesi itatajwa tena februal 27 mwaka huu

mwisho
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages