Breaking

Tuesday 10 January 2023

SERIKALI YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MLIPUKO



Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko kwa ajili ya watumishi wanaotoa huduma za afya na wateja wanaowahudumia,kutoka serikali ya Uingereza.

Makabidhiano ya vifaa hivyo yamefanyika Bohari ya Dawa (MSD) Keko Dar es Salaam,ambapo Mganga Mkuu wa serikali Prof. Tumaini Nagu amepokea vifaa hivyo kwa niaba ya serikali kutoka kwa Mkurugenzi wa Maendeleo wa ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Kemi Williams.

Akipokea msaada huo Prof. Nagu ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa vifaa hivyo na kueleza kuwa vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ni muhimu ili kupunguza hatari ya watoa huduma kuambukizwa wanapotekeleza majukumu yao.

Vifaa hivyo vitasambazwa na MSD kama Wizara ilivyoelekeza.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages