Breaking

Thursday 23 February 2023

MWANAFUNZI AMUUA MWALIMU KWA KUMCHOMA KISUMwalimu mmoja ameuawa mikononi mwa mwanafunzi wake ambaye alimshamubulia kwa kisu katikati ya somo.

Katika tukio hilo la Jumatano, Februari 22, lililotokea magharibi mwa Ufaransa, mwalimu huyo wa Kihispania mwenye umri wa miaka 52, alikuwa akifundisha darasani wakati mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16, alipomshambulia kwa kisu.

Shirika la habari la AFP likinukuu ripoti ya gazeti la Sud Ouest, lilisema kuwa mvulana huyo aliingia darasani wakati wa somo la Kihispania la mwalimu huyo.

Mwanafunzi huyo alifunga mlango wa darasa hilo kwa ndani na kumchoma kisu mwalimu kifuani mwake.

Kisha mwalimu huyo wa kike alifanyiwa huduma ya kwanza lakini alifariki kutokana na majeraha aliyopata huku mwanafunzi huyo akikamatwa na kwa sasa anazuiliwa kwenye seli ya polisi.

Vyombo vya habari nchini humo vilinukuu chanzo kikisema kuwa mvulana huyo alimwambia mwalimu mwingine kuwa sauti ilimwambia atekeleze kitendo hicho.

Kufuatia tukio hilo katika Shule ya Saint-Thomas d'Aquin, wanafunzi wote walizuiliwa kwenye madarasa yao kwa takriban saa mbili kabla ya kuruhusiwa kuondoka taratibu.

Wazazi waliokuwa wakiruhusiwa kuingia shuleni humo ni wale ambao wanao walikuwa katika darasa lililokuwa eneo la tukio.

Via: Tuko News
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages