Breaking

Thursday 23 February 2023

MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO ZINATUMIKA VIZURI-RC TABORANa Lucas Raphael,Tabora

Mkoani wa Tabora umeridhishwa na fedha zanazotolewa na serikali kwa ajili ya kutekelezaji wa miradi mbalimbali ya mendeleo kwa wananchi na kuchocheoa kasi ya kukuza uchumi wa mkoa huo.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian wakati akishuhudia utiaji saini kati ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Tabora Tuwasa na kampuni ya Peritus Eixm Private Ltd ya Dar –Es-Salaam kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kujenga Mabwawa ya kutibu Majitaka utakaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 1.6 uliofanyika ofisi za mamlaka hiyo jana.

Alisema kwamba fedha nyingi zinatolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya miradi ya maendeleo mkoani hapa inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na kutaka mradi huo usimamiwe kikamilifu.

Balozi Dkt Batilda alisema kwamba Mpango wa Serikali kupitia Wizara ya Maji ni kujenga mfumo mkubwa wa uondoshaji majitaka katika Manispaa ya Tabora.

Alisema kwamba Mradi huo utajumuisha ulazaji wa mabomba ya kukusanya Majitaka ,ujenzi wa Mabwawa ya kutibu majitaka kwenye maeneo ya Mansimba (nyuma ya Airport) na Kitongoji cha Igange kata ya Malolo ambapo . Maeneo hayo tayari yametengwa na Manispaa kwa ajili ujenzi wa mabwawa makubwa ya kutibu Majitaka katika Manispaa ya hiyo.

Awali Akitoa taarifa wakati wa utiaji saini Mkurugenzi Mtendaji wa Tuwasa Mhandisi Kashilimu Mayunga alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni kuongezeka kwa uzalishaji wa majitaka katika Manispaa hiyo, unaokadiriwa kuwa wastani lita 19,500,000 kwa siku baada ya wakazi wengi kuunganishiwa huduma ya maji ya mradi mkubwa wa kutoka ziwa Victoria.

Alisema kwamba Mradi huu unaogharimu shilingi Bilioni 1.6 unaunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha usafi wa mazingira katika Manispaa ya Tabora na hivyo kuboresha afya za Wananchi.

Mwakilisha kutoa wizara ya maji mhandisi mkuu Loishiye Ngotee alisema kwamba mradi hiyo itakapokamilika ya uondoshaji wa majitaka majumbani katika miji kumi ya Tanzania bara inaweza kufikia asilimia 30 kutoka asilimia 16 ifikapo mwaka 2025

Mkurungenzi Mtendaji kampuni ya Peritus Exim Pvt Ltd Triporari Goyal aliweleza mkuu wa mkoa wa Tabora kwamba wataukamilisha mradi huo ndani ya mktaba wa miezi 12 ila kikubwa wanaomba ushirikiano kutoka serikali ya mkoa wa Tabora .Mwisho
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages