Breaking

Wednesday 1 February 2023

WATU NANE WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI



Watu wanane wameuawa kwa kupigwa risasi wakisherehekea siku ya kuzaliwa katika boma moja nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Huduma ya Polisi wa Afrika Kusini (SAPS), wanaume wawili waliojihami kwa bunduki waliingia bomani humo na kuanza kufuatia risasi.

Watu waliokuwa wamekusanyika katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mmoja wao walimiminiwa risasi wanane wao wakiaga dunia na watatu kuachwa na majeraha.

Kisa hicho kilifnayika katika jiji la Port Elizabeth kusini mwa Afrika Kusni na uchunguzi wa kina umwanzishwa na polisi, washukiwa hao wakilenga kukamatwa.

Msemaji wa polisi wa Afrika Kusini Colonel Priscilla Naidu aliambia shirika la habari la CNN kuwa mwenye boma hilo ni mmoa wa waliouawa.

Taarifa ya SAPS inasema kuwa miongoni mwa waliouawa ni wanawake watatu na wanaume wanne.

Taraifa hiyo inaongeza kuwa hakuna mshukiwa yeyote aliyekamatwa kufikia sasa kuhusiana na kisa hicho.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages