Breaking

Saturday 11 February 2023

WATU WATATU WAUAWA KWA KIPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI




Mashambulizi ya wezi wa mifugo yameongezeka katika njia mbalimbali zinazoelekea na kuzunguka kaunti ya Turkana nchini Kenya. 

Mnamo Alhamisi, Februari 9, watu watatu waliuawa na mmoja kujeruhiwa vibaya katika shambulio la majambazi katika eneo la Kakong.

Majambazi hao wanaripotiwa kuvizia matatu iliyokuwa ikielekea Lodwar kabla ya kuinyunyiza kwa risasi.

Ili kuepusha vifo zaidi, dereva aliendesha gari kwa mwendo wa zigzag mbali na washambuliaji ambao walikuwa wamejifanya kama abiria.

Dereva Ishmael Wekesa alisema awali alidhani walikuwa wenyeji ambao walikuwa wamekwama akiongeza kuwa ilikuwa ya kushangaza alipokosa kuona mifugo barabarani.

“Sikuwa najua kama ni wahalifu lakini ile ng’ombe inakuwanga kwa barabara hatukuwa tunaona, wakati walipiga risasi ya kwanza juu, nikaona hapa siwezi simama ni kujiokoa, nikaendesha gari kwa mwendo wa zig zag...walipiga zingine na wakapata gari,” alisema.

Miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo lililosababisha mtu mmoja kujeruhiwa vibaya ni mwanafunzi wa shule ya upili, na mkimbizi anayesoma Kitale.

Kamanda wa polisi kaunti ya Turkana Samuel Ndayi alithibitisha kisa hicho na kuongeza kuwa maafisa zaidi wa polisi wametumwa kushika doria eneo hilo na kuzima mashambulizi zaidi.

Alitaja sehemu kati ya Kakong na KWS kuwaeneo hatari zaidi kwenye barabara kuu ya Kitale - Lodwar.

Hili likiwa ni tukio la nne katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja, wakaazi hao wameitaka serikali kuongeza polisi zaidi katika eneo hilo.




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages