Breaking

Saturday 11 February 2023

PANYARODI WAJERUHI WATU KWA MAPANGA DAR, WANNE WAKAMATWA



Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam lina washikilia watu wanne kufuatia tukio la vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa kundi la Panyarodi kuvamia makazi katika eneo la Bunju B Mtaa wa Idara ya Maji saa 8 usiku wa kuamkia Februari 10, 2023.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dr es Salaam, Jumanne Muliro amesema kundi la watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya wanane, walifika kwenye mtaa huo wakipiga kelele za mwizi, mwizi, ambapo nyumba zilizokuwa zinafungua wakifikiri ni wezi walikuwa wakivamiwa na kujeruhiwa.

“Ni kweli tukio kama hilo lipo, kikundi cha wahalifu walivamia kwenye mtaa huo, kama unavyojua nyumba moja ya kupanga iliyokuwa na familia zaidi tano ndio ilivamiwa, kwa hiyo sio nyumba nyingi zilizovamiwa kama wanavyoeleza.

“Kwa wale waliofungua walijeruhiwa huku wakiwaamuru watoe fedha na wale wasiotoa walijeruhiwa maeneo mbalimbali ya na kusababisha watu nane kupata majeraha ambapo waliikimbizwa hospitali,” alisema Muliro.

Kamanda Muliro amebainisha kuwa pamoja na watu kujeruhiwa vijana hao walisababisha uharibifu ikiwemo kupasua runinga kwa watu wasiokuwa na fedha.

“Baada yaku kupiga kelele vijana hao walichukua bajaji na kukimbia lakini baadae walikimbizwa na bodaboda, walipofika njiani waliruka na kukimbia, polisi walifika na kuanza msako ambapo vijana wanne walikamatwa, ingawa wawili walijeruhiwa vibaya.

“Upelelezi wa awali unaonyesha vijana hao wametoka Mkoa wa Pwani tunaenelea na uchunguzi. Tunawashauri viongozi wa mitaa hiyo kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi,”alisema

Soma zaidi >>HAPA

Via: Mwanachi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages