Breaking

Thursday 2 March 2023

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AFANYA MAZUNGUMZO NA WATANZANIA WAISHIO AZERBAIJAN

 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 02 Machi 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na watanzania waishio nchini Azerbaijan, Mazungumzo yaliofanyika katika Jiji la Baku nchini humo.

 
Kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya Makamu wa Rais leo March 02, 2023 imeeleza kuwa Makamu wa Rais amewaasa watanzania hao kuendelea kuitangaza vema Tanzania na vivutio vyake vilivyopo,kutangaza lugha ya Kiswahili na kuendelea kueneza utamaduni wa Tanzania pamoja na kuwa wazalendo kwa nchi yao. Pia amewaagiza kutoa elimu kwa watanzania wengine juu ya fursa za elimu zilizopo katika jumuiya yan chi wanachama zisizofungamana na upande wowote.
 
Makamu wa Rais amewataka watanzania waishio nje ya Tanzania kufuata sheria na taratibu za nchi walizopo pamoja na kujifunza mazuri katika nchi hizo na kuhamishia maarifa hayo nchini Tanzania. Pia amewaasa kutambua jukumu la kwanza la ujenzi wa Tanzania litafanywa na watanzania wenyewe hivyo wanapaswa kutoa mchango wa kila hali katika kuliletea taifa maendeleo.
 
Amesema serikali itaendelea kuleta mabadiliko yenye tija kwa watanzania wote ikiwemo kuendelea na jitihada za kuboresha sekta mbalimbali kama vile Afya, Elimu na Miundombinu pamoja na hivi sasa kuanzisha programu maalum ya kilimo ya Building Better Tomorrow itakayowasaidia vijana katika sekta hiyo.
 
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Mheshimiwa Fredrick Kibuta.
 
Makamu wa Rais yupo nchini Azerbaijan kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (Non-Aligned Movement) unaojadili kuhusu namna ya kukabiliana na athari za Uviko-19.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages