Breaking

Thursday 2 March 2023

MAMA AMNYONGA MTOTO WAKE WA MIAKA TISA


Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya, linamshikilia Regina Issack (40), anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili, mkazi wa Ilindi, Kata ya Ilemi jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake, Sisela Ngailo (09).


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea Februari 23, 2023 majira ya saa 7:00 mchana ambapo Regina alimnyonga shingo mwanae akiwa amelala.

"Chanzo cha tukio hili inasadikika mtuhumiwa kuwa na tatizo la afya ya akili ambapo alikuwa akihudhuria matibabu ya afya katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) tayari uchunguzi wa tukio hili unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika," amesema Kamanda Kuzaga.

CHANZO - EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages