Breaking

Saturday 11 March 2023

MUME AMUUA MKE NA KUMFUKIA CHUMBANI


Na Lucas Raphael,Tabora

Katika hali isiyokuwa ya kawadia mwanaume mmoja amemuuwa mkewe na kuchimba shimo  ndani ya chumba wanacholala na kumfukia humo na kulisakafikia kwa zege kutokana na madai ya wivu wa mapenzi .

 

Kauli hiyo ilitolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Richard Abwao alipokuwa akizungumza na  vyombo vya habari ofisini kwake jana ( Leo).

 

Alisema kwamba tukio hilo la mauaji liligundulika  machi 7 mwaka huu majira ya saa 9.30 aliasiri katika mtaa wa mbilani kata ya Kidongo Chekundu Manispaa ya Tabora na mkoa wa Tabora na Michael Hendry baada ya  kuona siku kadhaa zimepita bila chumba hicho kufunguliwa hivyo wakalazimika kuvunja mlango wa chumba cha kulala na kukuta chini ya kitanda kuna zege   ilikiwa  bado bichi alijakauka vizuri.

 

Alisema kwamba baada ya kuona hivyo alipata hofu iliyopelekea kufukua eneo hilo na kukuta mwili wa mtu umezikwa kwenye shimo hilo.

 

Kamanda Abwao  alimtaja alifariki na kuzikwa ndani ya chumba chake cha kulala  ni Salima Hamisi Maulidi (34)  na chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

 

Alisema kwamba mtuhumiwa baada ya kutekeleza unyama huo alimbia na jitiada za jeshi la polisi linaendelea kumsaka  na kuwataka wananchi wema ambao wanafahamu muuaji alipo watoe taarifa kwa jeshi la polisi ili kufanikisha kumkamata na kisha kufikisha kwenye vyombo vya sheria ili  kujibu mshitaka yanayomkabili .

Mwisho.   

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages