Breaking

Thursday 2 March 2023

MWANAUME AKAMATWA NA POLISI KWA KUJIFANYA MWANAMKE


Maafisa wa polisi wamemkamata mwanamume aliyekuwa akijifanya mwanamke katika soko la Bomet. 


Katika video iliyopakiwa kwenye TikTok na Noah Kips, mwanamume huyo alikuwa amevaa wigi iliyomfanya aonekane kama mwanamke. 


Pia alikuwa amevaa sidiria ambayo aliitoa baada ya maafisa wa polisi kumvamia. Maafisa hao wa polisi pia wanaonyeshwa wakimshurutisha kijana huyo kuvaa wigi lake vizuri na sidiria ili kumpa mwonekano mzuri wa kike. 


"Weka wigi lako hivi ili uonekane mwanamke. Chukua sidiria yako uvae na weka mifuko ya kazi ndani kama kawaida, iweke jinsi ilivyokuwa ili tukusamehe," maafisa hao. walimwambia mwanamume huyo. 


Kama inavyoonekana kwenye video, kijana huyo hakuwa na budi ila kufanya kama maafisa walivyoamuru. Hivyo, alitoa fulana yake ya pinki na kuvaa sidiria yake tena. 


Maafisa wa polisi walibaki wakishangaa na kumuuliza kwa nini alijifanya mwanamke. 


"Nia yako ilikuwa nini?" polisi mmoja alisikika akimuuliza lakini hakujibu. 


Maafisa hao walisikika wakimuuliza mwanamke aliyekuwa na mwanamume huyo sokoni iwapo alijua alikuwa mwanamume. Lakini mwanamke huyo alikana. 


“Sikujua, sisi sote tunauza bidhaa zetu hapa,” alisikika mwanamke huyo akimjibu afisa huyo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages