Breaking

Saturday 4 March 2023

WATU WAWILI WAFARIKI, MMOJA AJERUHIWA AJALI YA BAJAJI NA LORI


Watu wawili wamefariki  Dunia huku mmoja  akijeruhiwa baada ya Bajaji waliokuwa wamepanda kugongwa na Lori .


Ajali hiyo imetokea asubuhi ya Leo majira ya Saa 2 eneo la Mlima Ipogolo mjini Iringa baada ya Lori kufeli breki na kugonga Bajaji mbili .


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amethibitisha kutokea Kwa ajali hiyo na kuwa wanafuatilia zaidi eneo la ajali ili kujua ibadi sahihi ya vifo .


Kwa upande wake mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa Dkt Alfred Mwakalebela amesema kuwa awali walipokea Maiti mmoja ya kijana wa miaka 27 hivi na Majeruhi wawili wakiwa hoi na kati ya Majeruhi hao mmoja alifariki wakati akipatiwa matibabu na Majeruhi aliyebaki yupo ICU hali yake ni mbaya Sana .


Chanzo - Matukio Daima

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages