Breaking

Thursday 25 May 2023

BARABARA APP YATINGA BUNGENI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Moshi Kakoso (Kushoto), akipata elimu ya matumizi sahihi ya mfumo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya kutoka kwa Eng. Jacob Mukasa wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Bungeni jijini Dodoma.
Mbunge wa Bunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Fransis Ndulame (Kushoto), akisalimiana na Kaimu Meneja Mfuko wa Barabara Eng. Rashid Kalimbaga wakati wa zoezi la utoaji elimu ya matumizi sahihi ya mfumo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara inayotolewa na Bodi ya Mfuko wa Barabara, Bungeni jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Abbas Tarimba akitoa maoni yake kuhusu matumizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa hali ya barabara katika banda la Bodi ya Mfuko wa Barabara Bungeni jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Pastory Ushindi, Comfort Mgarula pamoja na Segolena Francis wote kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara.
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Zuberi Kuchauka akipakua Barabara App kwenye simu yake baada ya kupata elimu ya matumizi ya mfumo huo inayotolewa na Bodi ya Mfuko wa Barabara, Bungeni jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Segolena Francis na Comfort Mgarula kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara.
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Eng. Leonard Chamuriho (kushoto) na Eng. Mwanaisha Ulenge (kulia), wakitoa maoni yao baada ya kupata elimu ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara inayotolewa na Bodi ya Mfuko wa Barabara, Bungeni jijini Dodoma. Wengine ni Eng. Jacob Mukasa (kushoto kwa Chamuriho) na Msitiri Malongwe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.
Picha ya pamoja na watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wakati Bodi hiyo ikitoa elimu ya matumizi sahihi ya mfumo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara, Bungeni jijini.

Picha na Bodi ya Mfuko wa Barabara


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages