Breaking

Saturday 27 May 2023

KAMATI YA WAZIRI MKUU KUTEMBELEA MIKOA YOTE BARA NA VISIWANI

Kamati maalum ya kutatua changamoto za kibiashara nchini iliyoundwa na Waziri Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Khasim Majaliwa Majaliwa mapema leo tarehe 27 Mei, 2023 imehitimisha kazi ya kukusanya maoni ya wafanyabishara kutoka sekta mbali mbali Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Kamati hiyo DR.John Jingu amesema kuwa kamati hiyo imeshafanya kazi yake kwa asilimia sabini (70%) na sasa kamati inatawanyika katika makundi mbalimbali katika mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar ili kuwafikia wafanyabiashara waliopo katika maeneo hayo.

DR.Jingu amesema leo ikiwa ni siku ya tisa tangu kamati ianze kazi kuna baadhi ya changamoto za kiutendaji ambazo mpaka sasa zimeshatatuliwa kama mizigo ya baadhi ya Wafanyabiashara iliyokuwa ikishikiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeachiliwa na kusitishwa kwa vikosi vya operasheni za ukusanyaji kodi kwenye soko la Kariakoo.

“ wafanyabiashara wameshachukua mizigo yao na wengine wanaendelea kushughulikia jambo hilo ambalo limeleta matumaini kwa wafanyabiashara, tunashukuru kwa ushirikiano mkubwa kwa wadau wetu na wote tunaowatembelea wanatuambia tusimwangushe Mama’’ aliongeza Dr. Jingu.

Kwa upande wake Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo Bw.Hamis Livembe ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kwa kuwajumuisha kwenye kamati hiyo jambo linaloonesha Serikali ya awamu ya sita ni sikivu.

‘’Mara nyingi tumekuwa nje ya vyombo vya maamuzi lakini kwa sasa tunashirikiana na Seerikali kutatua changamoto za wafanyabishara nchini’’ alisisitiza Bw.Livembe.

Kamati hiyo inatagawanyika katika kanda tano ambazo ni Kanda za nyanda za juu kusini(Mikumi,Iringa,Makambako ,Mbeya na Tunduma), Kanda ya ziwa(Kahama ,Mwanza na Sirari), Kanda ya Pwani (Zanzibar, Lindi na Mtwara) Kanda ya Magharibi(Kigoma na Kagera) na Kanda nyingine ni Kanda ya Kaskazini yenye Mikoa ya Arusha , Kilimanjaro na Manyara.

Kamati hiyo inaundwa na wajumbe 14 ambapo wajumbe saba ni wawakilishi wa wafanyabiashara nchini na wajumbe wengine ni Kutoka idara na Wizara mbali mbali zinazohusika na biashara nchini.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages