Breaking

Thursday 18 May 2023

KONDA AUWA ABIRIA KISA AMEPUNGUKIWA NAULI, DALADALA YACHOMWA MOTO



Ukisoma kichwa cha habari unaweza ukashtuka lakini ndio ukweli kwamba konda amekatisha uhai wa abiria wake aliyepungukiwa nauli huko nchini Kenya.


Tukio hilo limetokea jana Jumatano Mei 17 katika Barabara ya Outering iliyoko jijini Nairobi, ambapo mzozo uliibuka kati ya konda na abiria huyo mwenye umri wa miaka 17 aliyepungukiwa kiasi cha nauli cha KSh 20.


Inadaiwa mabishano yalizidi kati ya konda na abiria huyo hivyo konda akaamuwa kumtupa nje wakati gari hilo likiwa kwenye mwendo, kwa bahati mbaya gari hilohilo ndilo lililomkanyaga na kumuuwa.


Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko ya nchini humo imesema konda huyo alichanja mbuga baada wakazi na wapiti njia wa eneo hilo kuamua kulichoma moto gari hilo.



Via: Mwananchi

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages