Breaking

Monday 6 May 2024

UDHIBITI UPOTEVU WA MAJI MBEZI MAKABE

Kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika bomba la inchi 8 lililoathiriwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katik eneo la Mto Lubomwe imetekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA)

Kukamilika kwa kazi hii kumeimarisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Makabe polisi, Makabe serikali ya Mtaa, Kwa Washa, Efatha, Msamaria, Kwa Mzungu, Kwa Biligenda, Dubai, Nyota njema na Kwa Fungo wilaya ya Ubungo.

DAWASA inaendelea kuwasihi wananchi kutoa taarifa endapo watabaina uvujaji katika maeneo yao mawasiliano rasmi ya Mamlaka kupitia Kituo cha huduma kwa wateja kwa 0800110064(bure) na mitandao ya kijamii.




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages