Breaking

Thursday 15 June 2023

AUAWA KWA KUCHOMWA KISU AKIDAI DENI LAKE

Familia moja ya Kirinyaga imeachwa katika huzuni baada ya kifo cha jamaa wao mwenye umri wa miaka 25, ambaye anadaiwa kudungwa kisu na kuuawa wakati akidai deni lake. 


Mamake, ambaye hakuweza kustahimili uchungu wake, alionekana akidai majibu jinsi mwanawe alivyokutana na kifo chake kisichotarajiwa. 


Katika video iliyoshirikishwa na Citizen TV, mwenzake alikwenda kumfariji baada ya janga hilo lililotokea Kagia, Kerugoya nchini Kenya. 


 "Nimekuja hapa kumfariji mwenzangu ambaye mwanawe aliuawa. Anadaiwa kuuawa na marafiki zake. Na tunataka haki kwa mwana huyu kijana. Tunataka suala hili la dawa za kulevya lifanyiwe uchunguzi kwa sababu alikufa akidai pesa zake," alisema 


Via: Tuko News

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages