Breaking

Monday 12 June 2023

MWANAKWAYA AIBA VIFAA VYA MUZIKI KANISANI, ATAKA ALIPWE KUVIREJESHA

Kanisa la Restoration International Churches huko Syokimau nchini Kenya limepoteza vifaa kadhaa vinavyotumiwa wakati wa sifa na ibada. 


Kevin Otieno Ngaira alijiunga na kanisa mapema mwaka huu na kuwa mwanachama wa kwaya. 


Baada ya kuelezea changamoto zake za kifedha, Askofu wa kanisa, Bwana Isindu, alihamasisha wanachama kadhaa kumsaidia kujiimarisha tena maishani.


 Miongoni mwa vitu alivyopokea ni kitanda, godoro, na vitu vingine vya nyumbani, pamoja na ruzuku ya kila mwezi ya KSh 10,000 kutoka nyumba ya Mungu kwa ajili ya mahitaji yake. 


Ni hatua ambayo walijutia muda mfupi baadaye walipogundua kwamba mwanaume huyo alikuwa na njama ya wizi. 


Alhamisi, Juni 8, Ngaira alirudi kwenye ghala la kanisa, akachukua funguo na kuondoka na keyboard ya Yamaha PSR670, mixer, na microphones kadhaa. 


Baada ya kuiba vifaa hivyo, Ngaira alianza kuwasiliana na wanachama wa kanisa akiomba pesa ili avirudishe. 


Kupitia ujumbe mrefu uliotumwa kwenye kikundi cha WhatsApp cha kanisa, alikiri kujuta kwa vitendo vyake lakini akasema maisha yalimfikisha katika hali hiyo. 


"Nilichukuwa keyboard na mixer na microphones, nia yangu haikuwa kuuza lakini nilitaka tu pesa kidogo ambayo ingenisaidia na ningezirudisha," alisema.

 

Hata hivyo, alianza kucheza mchezo wa kujificha wakati kanisa lilijaribu kuwasiliana naye na kukusanya vifaa vilivyopotea. 


Wakati wakiendelea na uchunguzi wa kisa hicho, ilibainika kuwa Ngaira tayari alikuwa ameuza vitu vya nyumbani alivyopewa kama sadaka. 


Baada ya kuandika ripoti katika kituo cha polisi, Ngaira alipewa siku tatu kurejesha vifaa hivyo kwa ahadi kwamba kesi ingefutwa, lakini hadi sasa hajafanya hivyo. 


 "Hatutamlaani kwa sababu alihudumu kwenye mimbari yetu, lakini wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba atajiunga na kanisa lingine na kufanya kitu kama hicho," aliongeza askofu. 


Wakati wa kuandika ripoti hii, kijana huyo alikuwa bado akiwasiliana na baadhi ya wanachama ili kuomba fedha zaidi. 

Via Tuko News

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages