Breaking

Friday 4 August 2023

RC MTAKA AIPONGEZA e-GA KUHAKIKISHA TAASISI ZA UMMA ZINATOA HUDUMA KIDIGITALI


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka, ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa jitihada kubwa inazofanya za kuhakikisha Taasisi za umma zinatoa huduma 

Mtaka ametoa pongezi hizo leo, alipotembelea katika banda la e-GA kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Mbeya.

"Mimi niwapongeze sana,mmekuwa mkifanya kazi nzuri ya kuhakikisha Serikali inatoa huduma zake kwa urahisi kupitia mifumo ya TEHAMA, rai yangu endeleeni kuja na bunifu mbalimbali lakini pia mhakikishe Taasisi zinaungana", alisisitiza.

Aliongeza kuwa, kwa muda mrefu Mamlaka ya Serikali Mtandao imekuwa ikija na bunifu za mifumo mbalimbali ya TEHAMA inayorahisisha utendaji kazi na kufanya huduma za Serikali zipatikane kwa urahisi.

Afisa Habari Mwandamizi Mamlaka ya Serikali Mtandao, Rainer Budodi alisema kuwa, Mamlaka inatoa elimu kwa wananchi wanaofika katika banda hilo ili waweze kufahamu na kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA iliyotengenezwa na Mamlaka.  



Alisema kuwa, baadhi ya mifumo ya TEHAMA ambayo e-GA inatoa elimu kwa wananchi wanaotembelea katika banda hilo ni pamoja na Mfumo wa e-Mrejesho ambao unawawezssha wananchi kuwasiliana na serikali kidijitali, Mfumo wa ubadilishanaji taarifa serikalini (GoVESB), Mfumo wa huduma za serikali kupitia simu za mkononi (MGOV) pamoja na Mfumo wa ukusanyaji wa data na takwimu (e-Dodoso)

Budodi alimshukuru kiongozi huyo kutembelea banda la Mamlaka, na kuwasihi viongozi na wananchi wengine kutembelea banda hilo ili kujionea bunifu mbalimbali za mifumo ya TEHAMA inayotengenezwa na vijana wa kitanzania kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).

Mamlaka ya Serikali Mtandao e-GA kwa mwaka huu 2023 inashiriki Maonesho ya Kimataifa ya wiki ya wakulima (nanenane) ambayo kwa mwaka huu maonyesho hayo kitaifa yanafanyika jijini Mbeya.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages