Breaking

Saturday 5 August 2023

KERO YA MAJI: WANANCHI WAMTAKA MBUNGE KUNYWA MAJI MACHAFU



Wakazi wa mitaa ya Milupwa na Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelalamikia changamoto ya ukosefu wa maji ambapo inawalazimu kutumia maji yasiyo safi na salama.

Mbele ya Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi Augosti 4, 2023 wakazi hao wamesema eneo hilo halina bomba hata moja wanatembea umbali mrefu kwenda kuchota maji machafu.

"Kupitia wimbo wakiwa wamebeba chupa ya plastiki iliyo na maji yasiyo salama walimuomba kunywa maji hayo ishara ya kutatuliwa kero hiyo," amesema.

"Walisikika kwa sauti moja tunaomba unywe pombe hii uone ilivyo tamu," zilisikika sauti zao.

Joyce John mwananchi wa eneo hilo, amesema maji hayo yanawaathiri kiafya kwa kuwa wamekuwa wakiugua matumbo ya kuhara mara kwa mara na watoto wao.

"Tumekuja nayo makusudi anywe maana tunafahamu hawezi kunywa anaogopa, atusaidie kuisimamia serikali itatue changamoto hii," amesema Joyce.

Aidha Kapufi kabla ya kutolea majibu kero hizo akahitaji kupata ufafanuzi kuhusu ukosefu wa maji kutoka ofisi ya Mamlaka ya Majisafi mjini Mpanda (Muwasa).

“Yupo mwakilishi hapa naomba uwaeleze wananchi hii kero itapatiwa ufumbuzi lini ili wananchi waondokane na tatizo hilo?” ameeleza.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi mjini Mpanda, Rehema Nelson akataja mikakati miwili ya muda mfupi na mrefu ili kukabiliana na changamoto ya maji.../

Soma zaidi >>HAPA<<

Chanzo: Mwananchi


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages