Breaking

Friday 4 August 2023

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MKOANI MBEYA

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika Maonesho ya Nanenane kitaifa yanayoendea Mkoani mbeya katika viwanja vya John Mwakangale ambapo shirika limeendelea kutoa elimu ya Viwango kwa wazalishaji, wauzaji, waigizaji wa bidhaa na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza kwenye Maonesho hayo leo Augost 4, 2023 Meneja wa Kanda ya Kusini, Bw. Abel Mwakasonda amesema TBS katika maonesho haya imepata fursa ya kuwatembelea wazalishaji wote wa bidhaa ikiwa ni pamoja na wajasiriamali wadogo na wa kati ambapo wameelekezwa kuhusu taratibu za kuthibitisha ubora wa bidhaa.

Aidha amewataka wazalishaji wa bidhaa kufika kwenye banda la TBS lililopo kwenye Maonesho hayo ili waweze kupatiwa elimu ya namna bora ya uzalishaji pamoja na kufanya usajili wa majengo ya chakula na vipodozi.

Amesema kupitia Maonesho haya TBS imefanikiwa kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuangalia alama ya ubora kabla ya kununua bidhaa na umuhimu wa kuangailia muda wa matumizi wa bidhaa husika kabla ya kununua bidhaa.

“Kimekuwa na wafanyabiashara wajanja ambao huuza bidhaa hafifu ziziso na alama ya ubora na pia wanauza bidhaa zilizoisha muda wa matumizi kwa kuwadanganya wananchi kuwa kuna muda ziada ambao wanaweza kutumia bidhaa hizo bila madhara. Tunawaasa wananchi kusoma taarifa katika bidhaa husika na kufuata maelekezo pasipo kukubali kudanganywa na wafanyabiashara”

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages