Breaking

Monday 18 September 2023

Sanjay Dutt atua nchini kufanya Royal Tour

Na John Mapepele

Msanii maarufu duniani kwenye eneo la filamu kutoka nchini ambaye ana zaidi ya wafuasi milioni mia mbili katika mitandao yake, Sanjay Dutt leo Septemba 18, 2023 ametua kuanza Royal Tour hapa nchini.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokewa na Mkurugenzi wa Utalii nchini Dkt. Thereza Mugobi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Damasi Mfugale, bwana Dutt amesema ameamua kuja kutembelea vivutio vya utalii nchini kufuatia Filamu ya The Royal Tour iliyochezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuonyesha hazina ya utajiri wa vivutio vya utalii nchini.

"Naipenda sana Tanzania, naiona niifanye Tanzania kuwa nyumba yangu ya pili sasa baada ya kuitazama filamu ya The Royal Tour" amesisitiza Dutt

Aidha, amesema ameamua kuwa balozi wa kujitolea kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mitandao yake kutokana na mapenzi yake kwa Taifa la Tanzania.

Mkurugenzi wa Utalii nchini Dkt Thereza Mugobi amefafanua kuwa Tanzania imefarijika kupata ugeni wa msanii huyo maarufu duniani kutoka India eneo ambalo lina idadi kubwa ya watu takribani bilioni 1.4 ambao ni soko la kimkakati la Tanzania.

"Ujio wa Dutt ni faraja kwetu kwa vile tunatambua itasaidia kuwa vuta wageni wengi kutoka bara la Asia ambako yeye anawafuasi wengi" ameongeza Dkt. Mugobi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Damasi Mfugale amesema Serikali itaendelea kuwakaribisha watu maarufu duniani ili wasaidie kufikia azma ya kufikisha wageni milioni tano ifikapo 2025 na kuliingizia Taifa dola bilioni Sita za kimarekani.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages