Breaking

Monday 25 March 2024

DAWASA MAPINGA WAENDELEA KUUNGANISHA WATEJA WAPYA

Habari njema kwa wakazi wote wa maeneo ya Kiharaka, Kiembeni, Changuaela, Kerege, Kibosha, Mtambani na Kimele kuwa ofisi ya DAWASA Mapinga inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.

Pamoja na zoezi hilo, elimu mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za mawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.

Zaidi ya wateja 100 wanatarajia kunufaika na huduma ya majisafi.

Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja nambari 0800110064 (Bure) au 0735 202121 (WhatsApp tu) 0734 359622 (DAWASA Mapinga).



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages