SHIRIKA lisilo la kiserikali la Smile for Community(S4C) kwa kushirikiana na Legal Services Facility (LSF) leo limetangaa msimu wa tatu wa mbio za Run for Binti zinazotegemea kukimbia tarehe 25 May 2024 jijini Dar es Saalam.
Mbio za Run for Binti zinazoratibiwa kila mwaka zina lengo la kuweka nguvu na rasmilimali za pamoja katika kuwawezesha watoto wa kike kupata haki ya elimu na afya ya uzazi kwa kuhakikisha wanapata hedhi salama , mazingira bora ya kusoma.Kupitia mbio za mwaka jana wanafunzi wa shule za sekondari Nanyamba na Chawi katika Halmashauri ya mji Nanyamba walinufaika kwa kujengewa vyoo bora na vya kisasa huku wanafunzi wa kike wakipata taulo ili kulinda afya zao na kuwawezesha kuhudhuria vipindi darasani bila kukosa.
Akiongea wakati wa Kutangaza Mbio hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Bi Lulu Ng’wanakilala amesema “Katika utekelezaji wa mradi wetu wa upatikanaji wa haki nchi tumeona dhahiri kwamba wasichana na mabinti wadogo wanakabiliana na vizuizi visivyoweza kuzuilika na vinavyozuilika katika kupata elimu, huduma za afya, na haki zao za msingi. Na ndio maana LSF tukaona ni vyema mashirikiano hayo na Smile for Community pamoja na wadau mbalimbali ni muhimu katika tunapunguza vikwazo na kutengeneza njia mpya itakayochochea kuwa na jamii yenye haki na usawa hususani kwa watoto wa kike
Mbio hizi za Run for Binti tangu zianze zimekuwa na tija kubwa katika kuwaleta wadau pamoja kwa kuweka rasilimali fedha na nguvu ya pamoja katika kutatua changamoto za jamii. Kupitia mbio za mwaka jana tumewezesha ukaratabi na ujenzi na miundombinu ya vyoo na usambazaji wa taulo za kike na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti mashuleni na hivyo kuwawezesha wanafunzi zaidi ya 2500 katika shule za sekondari za Mtwara kunufaika. Aidha kupitia utoaji wa elimu tumeweza kuongeza uelewa kwa jamii juu haki ya afya na hedhi salama pamoja na kusughulikia Ukatili wa kijinsia unaowakumba watoto na kupelekea kupata mimba za utotoni na hivyo kukatiza ndoto zao”.
Akitangaza tarehe ya mbio kwa mwaka huu Mkurugenzi Mkuu wa Smile for Community , Flora Njelekela amesema “Smile for Community kwa kushirikiana na LSF inayofuraha kubwa kutangaza mbio za Run for Binti Msimu wa Tatu zinazotarajia kufanyika tarehe 25 Mei katika Viwanja vya Oyesterbay Jijini Dar es saalam , Mbio hizi zitashirikisha wakimbiaji wa Km 21, Km 10 na Km5 pia tutakuwa na mbio za baiskeli za KM 55.
Lengo kubwa la kukimbia kwa mwaka huu ni kuwezesha watoto wa kike kupata mazingira bora ya elimu pamoja na afya ya uzazi hivyo makusanyo ya rasilimali fedha yataenda kujenga na kuboresha miundombinu kwa kujenga vyoo katika shule za sekondari, kuboresha upatikanaji wa maji salama kwa kujenga visima mashuleni,Kuboresha hedhi salama kwa kusambaza taulo za kike zinazoweza kutumika tena kwa wasichana,Kuchangia katika juhudi za uhifadhi wa mazingira kupitia upandaji miti na kutoa elimu juu ya kujilinda na kushughulikia ukatili wa kijinsia”.
“Sisi Smile for Community waanzilishi wa mbio hizi tunaona fahari kuwezesha jamii katika maeneo ya pembezoni kupata afya ya Uzazi na hedhi salama lakini kupata elimu endelevu kazi ambayo kama Taasisi tumekuwa tukiitekeleza kupitia miradi yetu mbalimbali na pia kupitia mbio hizi za Run for Binti kila mwaka. Hivyo nito rai kwa wadua mbalimbali kutuunga mkono kwa kushiriki na kuchangia mbio hizo kwani kushiriki kwako kutawezesha kumlinda mtoto wa Kike na kutumiza ndoto zake . Wanufaika wa mbio hizi ni wanafunzi zaidi ya 10,000 wa shule tano sekondari za mkoa wa Lindi na Mtwara. Alisisitiza Njelekela.