Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains iliyopo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania wamesafiri kuelekea Jijini Nairobi nchini Kenya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (World Championship Debate and Public Speaking Tournaments) yatakayofanyika kuanzia Mei 9,2024 hadi Mei 13,2024.
Uongozi wa shule umeweka wazi kuwa msafara una jumla ya wanafunzi 25, ambapo Mratibu wa somo la Kiingereza ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains , Josephine Kinyunyi anasema kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya wanatarajia kupata ushindi katika mashindano hayo ya kidunia na kuendelea kuipa heshima na kuitangaza nchi ya Tanzania kimataifa.
"Tunaelekea nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (World Championship Debate and Public Speaking Tournaments) ambayo ni mwendelezo wa mashindano ya Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (Johannesburg Summer Holiday Open Debate and Public Speaking Tournaments ) yaliyofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini kuanzia Desemba 11 hadi 19, 2023 ambayo Savannah Plains tulishinda tukapata nafasi ya kushiriki mashindano haya ya Dunia, kwa hiyo tunaenda Kenya kwa ajili ya hayo mashindano",amesema Josephine.
"Tuna historia ya ushindi, hivyo tunatarajia ushindi kwa sababu tulivyoenda Afrika Kusini tulishinda Mwanafunzi Yolanda Thomas Henjelewe ambaye alikuwa mshindi wa kwanza kutoka Tanzania, mshindi wa tatu kutoka Afrika Mashariki na mshindi wa tano wa Afrika. Lakini pia katika 10 bora tulikuwa na wanafunzi wetu wanne kutoka Savannah. Baada ya mashindano tulipewa Tuzo ya The Best Speaker from Tanzania, the Third Speaker From East Africa, na Fifth Speaker from Africa na kwa ujumla tulipewa Tuzo ya The Best Public Speaking School from Tanzania (The Best Tanzanian School – The Johannesburg International Summer Holiday Open – SHO”, ameongeza Josephine.
Uongozi wa shule umeishukuru serikali, wazazi na jamii kwa ujumla kwa kuendelea kushirikiana na shule hiyo katika masuala mbalimbali.
Shule ya Sekondari Savannah Plains ni miongoni wa shule zinazofanya vizuri. Shule hii ya bweni ipo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga mkabala na barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza.
Michepuo inayotolewa Savannah Plains High School ni PCM,PCB, PGM, HGE, EGM, HGL,HGK, HKL na ECA.
Kwa Mawasiliano zaidi +255 742 555 550 / 0743919187/0742919198
Mratibu wa somo la Kiingereza ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains , Josephine Kinyunyi akielezea namna walivyojipanga kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (World Championship Debate and Public Speaking Tournaments) yatakayofanyika Jijini Nairobi Kenya kuanzia Mei 9,2024 hadi Mei 13,2024. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa somo la Kiingereza ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains , Josephine Kinyunyi akielezea namna walivyojipanga kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (World Championship Debate and Public Speaking Tournaments)
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains iliyopo Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga wakiwa shuleni kabla ya kuelekea Jijini Nairobi nchini Kenya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (World Championship Debate and Public Speaking Tournaments) yatakayofanyika kuanzia Mei 9,2024 hadi Mei 13,2024.
Mratibu wa somo la Kiingereza ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Lugha katika Shule ya Sekondari Savannah Plains , Josephine Kinyunyi (kulia) akiwa na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains wakiwa shuleni kabla ya kuelekea Jijini Nairobi nchini Kenya kushiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye hadhara kwa kutumia lugha ya Kiingereza (World Championship Debate and Public Speaking Tournaments) yatakayofanyika kuanzia Mei 9,2024 hadi Mei 13,2024.