Breaking

Monday 13 May 2024

ZIMAMOTO WAZINDUA NYUMBA ZA MAKAAZI NA MAGARI.

DODOMA.

Mei 13, 2024

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Mhandisi Hamad Masauni (Mb) amezindua Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji zilizopo Kikombo Jijini Dodoma.

Uzinduzi huo umefanyika sambamba na uzinduzi wa Magari 12 ya kuzimamoto, yakiwemo Magari mawili ya Ngazi yenye uwezo wa kufanya maokozi katika Majengo Marefu yenye urefu wa ghorofa10.

Akimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Mhandisi Masauni amempongeza Kwa hatua hiyo ya kulitazama Jeshi la Zimamoto Kwa jicho pekee sana nakuongeza Kwa kusema haijawai kutokea Kwa Jeshi hilo kupewa vitendea kazi vya kisasa kama hivyo.

Aidha, Mhe.Masauni kupitia hutuba yake amewataka Askari wa Jeshi hilo kuyatunza Magari hayo ili yadumu kwa Muda mrefu.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita Kwa kulijengea uwezo Jeshi hilo .
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages