Breaking

Wednesday 21 August 2024

DAWASA YAENDELEA KUIMARISHA MAHUSIANO NA WATEJA



Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetembelea Wateja Wakubwa, Binafsi na na Taasisi za Serikali kwa lengo la kuboresha huduma na kubaini changamoto zao na kubadilishana uzoefu ili kuongeza juhudi katika kuhudumia Jamii.

Akizungumza wakati alipotembelea wateja katika mitaa ya Kivukoni, Shaban Robert na Chimala kata ya Kivukoni, Meneja wa DAWASA Mkoa wa kihuduma DAWASA Ilala Mhandisi Honest Makoi ameeleza kuwa lengo la Mamlaka ni kutoa huduma bora inayokidhi matarajio wa wateja.

"Leo tumetembelea baadhi ya Taasisi za Serikali na binafsi zikiwemo, Hospitali ya Ocean Road, Tume ya Taifa ya Ushidani (FCC), Wakala wa majengo Nchini (TBA) Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Makumbusho ya Taifa na nyingine nyingi na tumefurahi kuona wanaridhika na huduma zetu na wameahidi kuongeza ushirikiano ili kuboresha zaidi" alisema Mhandisi Makoi

Kwa upande wake, Bi. Roberta Feruzi ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano na kutoka Tume ya Taifa ya ushindani (FCC) ikiwa ni sehemu ya Taasisi za Serikali zilizotembelewa ameipongeza DAWASA na kutoa wito wa kuzidi kuboresha zaidi huduma kwa wateja kwa kuongeza wigo kwa wateja kutoa mrejesho wa huduma Mamlaka ili panapohitajika maboresho ya kihuduma yafanyike.

"Nimefurahi DAWASA kutembelea Taasisi yetu leo ni jitihada kubwa lakini bado kuna haja ya kutoa elimu zaidi kwa wateja haswa haki zao na wajibu wao kwa Mamlaka" alisema Bi. Feruzi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages