Breaking

Tuesday 10 September 2024

ELIMU KWA JAMII KIJIJI KWA KIJIJI DAWASA CHALINZE



Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea na uelimishaji wa makundi mbalimbali ya kijamii juu ya utunzaji na uhifadhi wa Miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya huduma ya Majisafi pamoja na kusikiliza changamoto za kihuduma kwa Wananchi wanaohudumiwa na Mamlaka.

Elimu hii imetolewa kwa Wananchi wa cha Kijiji Manga kilichopo Wilaya ya Handeni , Mkoani Tanga ambao ni wanufaika na utekelezaji wa Mradi wa Maji Chalinze awamu ya tatu uliokamilika kwa asilimia 100.

Afisa Maendeleo ya Jamii DAWASA Bi.Elizabeth Eusebius ametumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi wa hatua mbali mbali zinazochukuliwa na Mamlaka katika kuimarisha huduma ya maji katika Kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kufunga pampu mpya na kuimarisha mfumo wa umeme wa njia tatu katika tenki la maji Tengwe.






Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages