Breaking

Thursday, 15 May 2025

AGGYBABY KUWANIA TUZO ZA KIMATAIFA – EAEA TANZANIA 2025

  iikm

Mrembo mahiri, maarufu na mwenye vipaji lukuki, Agness Suleiman almaarufu Aggy baby, ameandika historia mpya katika tasnia ya burudani na jamii baada ya kutangazwa rasmi kuwa miongoni mwa wateule wa Tuzo kubwa za Kimataifa za Africa Arts Entertainment Awards (EAEA) 2025, zinazotarajiwa kufanyika hapa nchini Tanzania.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa mitandao ya kijamii, Aggybaby ameandika kwa furaha:

"Nawashukuru sana kwa support zenu nyie mashabiki zangu 🙏 Hatimaye nimeingia kwenye tuzo kubwa ya kimataifa katika vipengele vingi ikiwemo Music, Maigizo pamoja na mambo ya kijamii 💎"

Aggybaby ametajwa katika vipengele vitano muhimu vinavyoonyesha upana wa vipaji vyake na mchango wake katika jamii:

✅ Actress of the Year

✅ Best Female Fashion Designer

✅ Best Inspirational Youth Icon / Motivator

✅ Best Upcoming Artist (Female)

✅ Founder of the Year (kupitia taasisi yake ya Tupaze Sauti Foundation)

Uteuzi huu ni ushuhuda wa kazi kubwa anayofanya Aggybaby si tu kwenye sanaa, bali pia katika kuhamasisha na kuinua vijana wa Kitanzania kupitia shughuli za kijamii na maendeleo.

Mashabiki na Watanzania kwa ujumla wanahimizwa kuendelea kumuunga mkono msanii huyu wa kipekee ambaye sasa ni nembo ya ubunifu, kipaji na uzalendo.

Aggybaby si tu msanii, bali pia ni kielelezo cha matumaini na uthubutu kwa kizazi kipya.

🔗 Fuata kurasa rasmi za tuzo hizi kwa taarifa zaidi:

@eaea\_tanzania na @eaea\_awards\_inc

 #AggybabyFahariYaTanzania 🇹🇿

 #EAEATanzania2025

*#TalantaZaKikwetu

 #EAEACountryLevelAwards2025

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages