Breaking

Thursday, 15 May 2025

Mke wa Rais Finland Afanya “Royal Tour” Makumbusho ya Taifa Dar

Na Mwandishi Wetu

Mke wa Rais wa Finland, Suzanne Innes-Stubb, leo Jumanne Mei 14, 2025, amefanya “Royal Tour” kwenye Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine alifurahia sana historia ya zamadam na utamaduni wa Tanzania.

Akipokewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo Dkt. Noel Luoga, Mama Suzanne Stubb, mtaalam wa sheria za Umoja wa Ulaya, ameeleza kufurahia historia ya zamadam na kueleza matamanio yake kwa watafiti kutoka nchini Finland kuja kujifunza zaidi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages