Breaking

Tuesday, 13 May 2025

SAVANNAH PLAINS SHINYANGA YANG’ARA MASHINDANO YA DUNIA YA MJADALA AFRIKA MASHARIKI

Mratibu wa somo la Kiingereza na Mkuu wa Idara ya Lugha Shule ya Sekondari Savannah Plains, Josephine Kinyunyi akizungumza.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains walioshiriki East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2025.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shule ya Sekondari Savannah Plains, iliyopo Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga, imeonesha uwezo mkubwa wa kielimu na kuitangaza vyema Tanzania katika anga za kimataifa baada ya kung’ara kwenye Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa Shule za Afrika Mashariki kwa Lugha ya Kiingereza (East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2025) yaliyofanyika kuanzia Mei 9 hadi 11, 2025, jijini Nairobi, nchini Kenya.

Katika mashindano hayo yaliyokutanisha zaidi ya 200 ya timu kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Savannah Plains imefanikiwa kushika nafasi ya tano barani Afrika na nafasi ya kwanza kwa Tanzania, ikiwakilishwa na timu ya wanafunzi 14 kutoka kidato cha kwanza hadi cha tatu.
Akizungumza leo Mei 13, 2025 mara baada ya kurejea shuleni na timu yake, Josephine Kinyunyi, Mratibu wa somo la Kiingereza na Mkuu wa Idara ya Lugha wa shule hiyo, amesema ushindi huo ni wa kihistoria na umelitangaza vyema jina la Tanzania katika ramani ya dunia.

“Tumerudi na kombe na medali, tumeiwakilisha vyema Tanzania. Timu zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali za Afrika zilishiriki mashindano haya. Kutoka Tanzania, shule saba ziliwakilisha nchi, na sisi Savannah Plains tumefanikiwa kuibuka washindi wa kwanza kwa upande wa Tanzania na nafasi ya Tano barani Afrika. Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata ushindi huu mkubwa, na pia tunaishukuru serikali kwa kuendelea kutuunga mkono,” amesema Kinyunyi.

Bi. Kinyunyi ameongeza kuwa sasa wanaanza mara moja maandalizi ya kushiriki mashindano ya kimataifa yatakayofanyika nchini Marekani, huku akieleza kuwa wanafunzi wao wamejengeka kimaadili, kiujuzi, na kiakademia kushindana kwenye majukwaa ya kimataifa.

Kwa upande wake, Deogratius Makoko, Mdhibiti Ubora wa Shule hiyo aliyemwakilisha Mkurugenzi wa shule, ametoa shukrani kwa serikali, wazazi, na jamii kwa ushirikiano wao mkubwa katika kuwawezesha wanafunzi kushiriki mashindano ya kimataifa.

“Huu ni ushindi wa taifa zima. Nafasi ya tano Afrika ni jambo la kujivunia. Tunawaalika wazazi wote wajiunge nasi kwa ajili ya elimu bora, maadili mema na maandalizi ya vijana wanaoweza kushindana duniani kote,” amesema Makoko.

Pongezi pia zimetolewa na Mkaguzi wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Joel Obadia, aliyesema kuwa Jeshi la Uhamiaji linaendelea kushirikiana na shule yoyote inayotaka kusafirisha wanafunzi nje ya nchi, huku akibainisha kuwa Tanzania ina uhusiano mzuri na mataifa mengine duniani.

Wanafunzi walioshiriki mashindano hayo wameonyesha furaha yao, wakiwemo Baraka Abdul, aliyefika hadi nusu fainali, na Allan Raymond pamoja na Abigail Imani Mgaya waliotinga hatua ya robo fainali.

Wote wameishukuru shule yao na serikali kwa kuwawezesha kushiriki na kuahidi kujitahidi zaidi kwenye mashindano yajayo.

Ushindi huu wa Savannah Plains ni ishara ya mafanikio ya mfumo wa elimu nchini na nguvu ya kushirikisha vijana katika majukwaa ya kimataifa, hasa katika kukuza uwezo wa kujieleza kwa lugha ya Kiingereza, mijadala na ujasiri wa kuongoza kwenye majukwaa ya kimataifa.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Savannah Plains walioshiriki Mashindano ya Ubingwa wa Dunia wa Mjadala na Kuongea kwenye Hadhara kwa Shule za Afrika Mashariki kwa Lugha ya Kiingereza (East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2025.
Mratibu wa somo la Kiingereza na Mkuu wa Idara ya Lugha Shule ya Sekondari Savannah Plains, Josephine Kinyunyi akizungumza baada ya kurejea shuleni na timu yake kutoka kwenye East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2025 jijini Nairobi, Kenya.

Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Savannah Plains ,Abigail Imani Mgaya akizungumza baada ya kutoka kushiriki kwenye East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2025 jijini Nairobi, Kenya.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Savannah Plains ,Baraka Abdul akizungumza baada ya kutoka kushiriki kwenye East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2025 jijini Nairobi, Kenya.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Savannah Plains, Allan Raymond akizungumza baada ya kutoka kushiriki kwenye East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2025 jijini Nairobi, Kenya.
Kombe la ushindi kwa Shule ya Sekondari Savannah Plains ilivyoshiriki East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2025
Plains ilivyoshiriki East Africa World Schools Debate and Public Speaking Championships 2025
Mdhibiti Ubora wa Shule ya Sekondari Savannah Plains, Deogratius Makoko akieleza furaha yake kuhusu ushindi wa shule hiyo

Mkaguzi wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Joel Obadia akieleza namna wanavyoshirikiana na mataifa mbalimbali kurahisisha wananchi kusafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine
Mkaguzi wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Joel Obadia akieleza namna wanavyoshirikiana na mataifa mbalimbali kurahisisha wananchi kusafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages