SERIKALI imeondoa Tozo ya Shilingi 100 kwa kila lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa, zilizopaswa kulipwa na watumiaji wa mafuta nchini kwa muda wa miezi mitatu zaidi kuanzia mwezi Machi 2022 hadi mwezi Mei 2022.
Hayo yameelezwa Kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara ya Nishati Kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Februari 28,2022;