Breaking

Tuesday 22 March 2022

RAIS SAMIA ATOA WITO UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Watanzania kutunza mazıngira, hususani uoto wa asili kwa kuepuka kukata au kuchoma miti ovyo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imesema kuwa Rais Samia  Rais ametoa wito huo leo wakati akihutubia katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Amesema katika maeneo ya vijijini, chemichemi nyingi za maji pamoja na baadhi ya mito imetoweka kutokana na uharibifu wa mazıngira, na pia kutokana na kufanya shughuli nyingine za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.


Aidha, Rais Samia ameielekeza Wizara ya maji kufanya utafiti na kuangalia uwezekano wa kutumia maji ya Mto Rufiji kwa ajili ya matumizi ya baadae katika jiji la Dar es Salaam.

Awali akizindua mradi wa maji uliogharimu shilingi Bilioni 18 utakaosambaza maji kutoka Mboga, Chalinze hadi Mlandizi Wilayani Bagamoyo, Rais Samia ameikopesha Wizara ya Maji shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi ili yaweze kuwafikia kwa haraka.

Amewataka wananchi kuhakikisha wanalipa ankara za huduma ya maji wanayopatiwa ili Mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Dar es Salaam (DAWASA) iendelee kutoa huduma kwao.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages