Breaking

Tuesday, 12 April 2022

CAG ABAINI MASHIRIKA 14 YALIYOPATA HASARA, MADAI 56 YALIYOONESHA WANAUME WALIJIFUNGUA



Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere ametaja Mashirika ya kibiashara yaliyopata hasara kwa miaka miwili 2019/20 na 2020/21.

Akizungumza wakati akiwasilisha Ripoti yake kwa waandishi wa habari leo Jumanne April 12,2022 ametaja mashirika 14 ya kibiashara yaliyopata hasara mfululizo.


CAG Kichere amesema hali hiyo ilisababishwa na hasara kwenye uwekezaji uliofanywa, ufanisi duni wa mashirika husika, na u
dhibiti hafifu wa mapato na matumizi.


Baadhi ya mashirika hayo kuwa ni ATCL, Mkulazi, TTCL, Kituo cha Mikutano Arusha, EPZA, Watumishi Housing na Kampuni ya Uchapishaji ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


"Naomba nifafanue kuhusu mwenendo Kampuni ya Ndege Tanzania, mwenendo wake umeimarika ukilinganisha na mwaka uliopita kwa sababu kwa mwaka 2020/21, kampuni iliongeza mapato kwa asilimia 11 na kupunguza matumizi kwa asilimia tatu" amefafanua


"Hivyo, Kampuni ilipunguza hasara ya jumla kutoka Sh. bilioni 60.25 mwaka 2019/20 hadi kufikia Sh. bilioni 36.18 mwaka 2020/21"

Aidha ameyataja Mapungufu ya udhibiti kwenye mfumo wa madai wa Mfuko wa Bima ya Afya ikiwemo madai 56 yanayoonesha Wanaume walipata huduma ya upasuaji (C/S) au huduma za kawaida za kujifungua wakati huduma hizi hutolewa kwa Wanawake.


Ameongeza kuwa Wanachama 444 waliopata huduma ya kuchunguzwa picha kamili ya damu (full blood picture) zaidi ya mara moja kwa siku moja (hadi mara 30) kwenye kituo kimoja.

"Aidha, kuwapo kwa malipo ya madai yaliyorudiwa, pamoja na madai yanayoonesha wanachama wa NHIF waliopokea miwani ya kusomea zaidi ya mara moja wakati utaratibu unaruhusu kutoa miwani mara moja kwa mwaka"

"Udhaifu huu umesababishwa na kukosekana kwa udhibiti katika mfumo wa madai iliyosababisha hasara ya Sh. Milioni 14.41 kwa mfuko"

"Ninapendekeza kwamba Mfuko wa Bima ya Afya: (a) Kurejesha kiasi kilichopotea kutoka kwa watoa huduma za afya husika; na (b) Kuboresha mfumo wa madai wa CMIS ili kuhakikisha kuwa unasaidia maafisa wanaohusika kuangalia uhalali wa madai yaliyowasilishwa"
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages