Breaking

Tuesday 12 April 2022

RAIS WA UKRAINE AOMBA KUHUTUBIA UMOJA WA AFRIKA (AU)



Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenksy ameomba kuhutubia Umoja wa Afrika (AU) kutokana na vita vinavyoendelea nchini humo ili kuwaeleza Waafrika jinsi vita hiyo itakavyo athiri Dunia.

Akithibitisha mazungumzo hayo Mwenyekiti wa AU, Macky Sall ambaye pia ni Rais wa Senagal amesema ombi hilo limekuja baada ya kuwa na mazungumzo na Zelenksy kuhusu madhara ya kiuchumi yatakayotokea kutokana na vita vinavyoendelea Ukraine.

Social embed from twitter



Rais Zelensky alimpigia simu Rais wa Senegal Macky Sall jana Jumatatu April 11, 2022 na mazungumzo yao yaligusia taarifa ya AU mwezi Februari iliyotaka kusitishwa mara moja kwa mapigano na kurejelewa kwa mazungumzo.

Katika mazungumzo hayo ya simu, Bw Zelensky alimfahamisha Bw Sall kuhusu "mapambano ya Ukraine dhidi ya uvamizi na uhalifu wa kutisha wa mchokozi wa Urusi", kulingana na ujumbe wa Twitter.

Social embed from twitter


Mataifa ya Afrika yameonyesha kutokuwa na umoja katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Senegal ilikuwa miongoni mwa nchi 17 za Kiafrika ambazo hazikupiga kura katika Umoja wa Mataifa kuhusu azimio la kutaka Urusi ikomeshe operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine. 

Social embed from twitter

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages