Breaking

Friday 13 May 2022

ASKARI UHIFADHI WALIODANGANYA KUVUNA MAMBA BUCHOSA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amemuelekeza Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii  kuwachukulia hatua za kinidhamu Askari wa Uhifadhi watakaothibitika kuidanganya Serikali kwamba wameshiriki katika zoezi la kuvuna mamba wawili Wilayani Buchosa Mkoani Mwanza.


Ameyasema hayo leo Ijumaa Mei 13, 2022 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Buchosa, Mhe. Eric James Shigongo kuhusu mikakati ya Serikali ya kuzuia mamba wanaoua watu Jimboni Buchosa.


Amefafanua kuwa Serikali katika kukabiliana na changamoto hizo, inaendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Migongano baina ya Binadamu na Wanyama wakali na waharibifu. 


Awali akijibu swali la msingi Mhe. Masanja alisema kuwa Serikali imevuna jumla ya mamba wawili katika wilaya hiyo.


“Kuanzia kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 jumla ya mamba wawili (2) wamevunwa Wilaya ya Buchosa".

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages