Breaking

Friday 13 May 2022

OPARESHENI PANYA ROAD YAENDELEA, WENGINE 23 WAKAMATWA DAR




Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watuhumiwa 23 kwa tuhuma mbalimbali za kihalifu huku wengi wao wakiwa ni vijana wanaojihusisha na matukio ya unyang'anyi ya kutumia nguvu na silaha aina ya mapanga na visu maarufu kama 'Panya Road'.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Saaam, ACP Jumanne Muliro amebainisha hayo Mei 12, 2022 wakati akizungumza na waandishi wahabari ofisini kwake, kama sehemu ya muendelezo wa operesheni kali inayoendelea usiku na mchana kupitia taarifa fiche,

Miongoni mwa watumiwa hao Kamanda Muliro amesema watuhumiwa 11 wamekamatwa baadaya kuvamia nyumba mbili katika eneo la Nyantila na kufanikiwa kuiba TV tatu na simu moja baada ya kuwajeruhi baadhi ya watu.

"Kufikia tarehe 11.5.2022 tayari wamekamatwaa Watuhumiwa 23 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha mapanga na visu , kuvunja nyumba usiku, kujeruhi na kuiba vitu mbalimbali hasa maeneo ya Kitunda, Mwanagati Ilala na Kinondoni maeneo ya Kunduchi Mtongani na Tegeta"


"Oparesheni hii ambayo ni endelevu inafanywa usiku na mchana na ilianza tarehe 27/04/2022 na imefanikiwa kuwakamata wahalifu hao ambao wengi wao wana umri kati ya miaka 13-24, katika mahojiano, Jeshi la Polisi limebaini kuwa baadhi ya Watuhumiwa hao hawakumaliza Shule ya Msingi kwa utoro na sababu zingine mbalimbali"

SomaPANYA ROAD 31 WAKAMATWA, WAKUTWA NA TV 12 NA SIMU 4

"Baadhi ya Watuhumiwa waliokamatwa walifanya tukio la unyang'anyi tarehe 10/05/2022, huku wakidai kulipa kisasi kwa baadhi ya Waty wa maeneo hayo baada ya Mtuhumiwa mwenzao kufariki kwa kushambuliwa na Wananchi wenye hasira kali kwa kujihusisha na wizi.

Katika hatua nyingine, Kamanda Muliro ameonya watu walioanza tabia ya kuzusha taarifa zinazoleta taharuki, ya kwamba kuna makundi ya 'Panya Road' yanaendelea na uvamizi, ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakipita maeneo mbalimbali na wakikuta vijana zaidi ya watano wanatuma ujumbe. kwamba wamekutana na 'Panya Road' na kuzusha taharuki. Tabia hiyo imejitokeza katika maeneo ya Bonyokwa, Kitunda na Charambe.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages