Breaking

Tuesday 28 June 2022

DC MKUDE AAGIZA MSAKO WAPIGA RAMLI CHONGANISHI "LAMBALAMBA" KISHAPU

Na Severn Mbullu, (LLH) Kishapu


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe, Joseph Modest Mkude Amepiga Marufuku kwa watu wanaopiga lamri  Chonganishi wanaojiita Lambalamba kuendelea na Shughuli zao wilayani Humo


Dc Mkude ameyasema hayo leo June 27,2022 katika Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya WIlaya ya Kishapu.

Amewataka Viongozi  wote wa Ngazi mbalimbali Kushirikiana na kuhakikisha  wanakomesha swala la Lambalamba ambalo linaleta uvunjifu wa Amani katika Wilaya hiyo.


"Watu hao hawakubaliki na mtu yoyote na hawajapata kibali cha mtu yoyote yule toka mahali popote. Kama kuna mtu anauhakika wana vibali amlete ofisi ya Mkuu wa wilaya mara moja ili aweze kuruhusiwa kuendelea na shughuli hiyo anayotaka kuifanya. Kwa wito huu ndugu viongozi wote katika ngazi mbalimbali ninaomba ushirikiano mkubwa ili tuwabaini watu hao na kutowakaribisha kufanya shughuli zao hizo potofu" amesema Dc Mkude


"Natoa wito kwa Uongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji hakikisheni mnatoa taarifa haraka juu ya uwepo wa watu hao ili hatua za Kisheria  zichukuliwe" Alisema Mhe, Mkude



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages