Breaking

Tuesday 28 June 2022

RC MJEMA AAGIZA HOJA ZA CAG HALMASHAURI YA MSALALA KUTATULIWA




Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema ametoa agizo la kuhakikisha hoja zote ambazo zimetolewa kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ya mwaka 2020/2021 katika Halmashauri ya Msalala zinafanyiwa kazi pamoja na kutatuliwa kwa haraka ili zifungwe.


Rc Mjema ametoa agizo hilo leo Juni 28,2022, kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa ya CAG.

Amesema mara kwa mara Halmashauri hiyo ya Msalala ambayo ipo katika wilaya ya Kahama imekuwa ikikabiliwa na mrundikano wa hoja nyingi za kujibu pamoja na kuzitatua Swala Ambalo Huifanya kupata hati ambayo ina mashaka mashaka licha ya Kuwa na Hati Safi .

Ameongeza kuwa mrundikano wa hoja hizo kutokufanyiwa kazi zinaisababishia Halmashauri pamoja na idara zake kuonekana hazisimamii utekelezwaji mzuri jambo ambalo yeye kama Mkuu wa Mkoa hayuko tayari kuona jambo Hilo likiendelea .


"Halmashauri hii inajitahidi kufanya vizuri na niwape hongera kwa kupata Hati safi lakini niwatake Sasa muhakikishe kila hoja ambayo imetolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali zinajibiwa zote na kusiwe na mara hoja za Miaka ya nyuma hazijafanyiwa kazi Wala kujibiwa huku mnasababisha mrundikano wa hoja katika Halmashauri hii" amesema Mjema

Aidha Rc Mjema amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kahama ambaye ndie mlezi na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama kwa Halmashauri hiyo na wilaya ya Kahama kuhakikisha wale wote ambao wamehusika na kutajwa katika Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali katika ubadhirifu wa fedha anawachukulia hatua haraka.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe.Festo Kiswaga amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kutekeleza agizo hilo lililotolewa sambamba na kuhakikisha kila idara inayohusika na hoja zilizotolewa basi zinatatuliwa na kukamilishwa kwa Wakati.

Naye Mkaguzi Mkuu wa nje wa Hesabu za serikali toka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Mkoa wa Shinyanga Bwn. Anselimu Faustine Tairo amesema kwa Halmashauri hiyo ya Msalala pamoja na kwamba inajitahidi katika makusanyo ya mapato lakini inapaswa kuhakikisha inatoa elimu kwa watumishi wake kuwa na uwezo wa kuandaa hoja pamoja na kuiwasilisha kwani wamekuwa wakipata tabu wakati wanapokuwa wanataka taarifa ya matumizi fulani wamekuwa hawapati maelezo ya kutosha.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages