Breaking

Wednesday 29 June 2022

TAASISI ZA UTAFITI ZAWEKA MIKAKATI YA UZALISHAJI WA MBEGU BORA



Mabadiliko ya Tabia Nchi yamezifanya Taasisi zinazozalisha Mbegu,zinazofanya tafiti na uthibiti ubora ziweke mikakati ya kuongeza uzalisha wa Mbegu bora za kilimo ilikukabiliana na Ukame.


Mabadiliko ya Tabia Nchi yamewafanya wadau katika Sekta ya Kilimo kukutana katika Kikao kazi Mkoani Morogoro Ili kuweka mikakati ya pamoja ya Uzalishaji Mbegu zinazokabiliana na ukame,



Kikao kazi hicho ambacho kimezikutanisha Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo zinazozalisha,kutafiti na kuthibiti ubora wa Mbegu ikiwemo ASA,TARI pamoja na TOSCI kilichofanyika Mkoani humo kinalenga kuongeza tija katika kilimo hapa nchini.





Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI Patrick Ngwediagi alizitaka Taasisi zote zinazofanya tafiti na kuzalisha Mbegu Nchini kuzingatia ubora wa Mbegu kwa kuzingatia viwango vya ubora unaotakiwa na Serikali.



Kwa mujibu wa Ngwediagi lengo la Taasisi ya uthibiti ubora wa Mbegu Nchini ni kuhakikisha kuwa Nchi inakuwa na Mbegu bora na zenye tija kwa Taifa ambazo zitamwezesha Mkulima kuzalisha mazao bora hali itakayosaidia kuongeza uzalishaji na hivyo kuongeza uchumi kwao na Taifa kwa ujumla.



Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafitia wa Kilimo Tanzania TARI Dkt Geoffrey Mkamilo alisema kuwa Taasisi zote tatu zinategemeana na kwamba endapo mmoja akikosekana basi swala la Mbegu linakuwa halijakamilika.



Dkt Mkamilo alisema kuwa Taasisi ya uthibiti ubora wa Mbegu imewasaidia wao Kama TARI pamoja na Wakala wa Mbegu za Kilimo za kilimo ASA kuhakikisha wanafanya tafiti na kuzalisha Mbegu ambazo zinaushiandani katika Soko la Mbegu Nchini.



"hata katika upande wa uthibiti TOSCI inahusika katikakushauri namna Bora ya kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na viwango vya ubora wa Mbegu unaohitajika"alisema



Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt Sophia Kashenge alisema kuwa Kama wadau waliona ni namna gani wakae Kama wadau wa Sekta hiyo Ili waone ni kwa namna gani wanaweza kujadili mwenendo, changamoto au fursa katika Uzalishaji mbegu Nchini.



Dkt Kashenge alisema kuwa Wizara imewapa kazi kubwa Sana na kwamba bajeti imeongezeka ambapo alisema kuwa moja ya Vipaumbele vinne katika wizara kimoja wapo ni Uzalishaji wa Mbegu na umwagiliaji na kwamba Uzalishaji wa Mbegu ni mkubwa lakini bado wanahitaji Tani nyingi zaidi Ili kukidhi mahitaji ya watanzania.



"mwaka Jana Uzalishaji ulikuwa Tani 800 mpaka 1400 wakati mahitaji ya mbegu kwa mwaka ni Tani 371,750"alisema



Mwisho.

 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages