Breaking

Tuesday 21 June 2022

WATATU WAKAMATWA KWA KUMLAWITI KISHA KUMUUA MTOTO WA MIAKA SABA - GEITA




Watuhumiwa watatu ambao ni Mathias Shilole (26) Mkulima, Sita Makabila (52) Mganga wa tiba asili na Mkazi wa Kilimanjaro Nyangwale, na Lucy Mdelema wamefikishwa Mahakamani kwa kosa la kumuua Mtoto Dorcas Mathias mwenye umri wa miaka 7 Mwanafunzi wa chekechea Shule ya Msingi Ibambila Wilayani Nyahg"wale Mkoani Geita.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema Watu hao watatu walimvamia Binti huyo aliyekuwa akichunga mbuzi na mwenzie na wakaondoka nae na kisha kumficha sehemu isiyojulikana na baadaye Watuhumiwa Wanaume wakambaka na kumlawiti na kumvunja shingo yake baada ya kumuua .

Mwaibambe amesema baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi wa Daktari ulibainika kuwa Dorcas alibakwa, kulawitiwa na kisha kuuawa na baadaye akavunjwa shingo.


Source: Millard Ayo
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages