Breaking

Tuesday 26 July 2022

DC MASALLA AKABIDHI MADAWATI 1500 SHULE ZA MSINGI ILEMELA



Mkuu wa Wilaya ya Ilemala Hassan Masalla amesema maendeleo yanayoonekana katika wilaya hiyo ni kutokana na wadau kuisaidia Serikali katika kusukuma gurudumu hilo la kuondoa changamoto zilizopo.

Ameyasema haya wakati akiyakabidhi jumla la Madawati elfu moja na mia tano ambayo yamewezeshwa na wadau wa maendeleo katika wilaya hiyo baada ya DC Masala kuandaa harambee ya kuchangia pesa za kutengeneza madawati.

DC Masala amewashukuru wadau wote waliochangia, na kusema kama Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wananchi wake ili kuwaletea maendeleo.

"Kazi wilaya tunayo malengo ya kimkakati ya kuyatekeleza, mimi pamoja na timu nzima ya uongozi wa wilaya tunashirikiana kuhakikisha tunayafikia" - Hassan Masala Mkuu wa Wilaya ya Ilemela.

"Haya yote tunayoyafanya ni katika kumsaidia Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya ya Ilemela" - Hassan Masala, Mkuu wa wilaya Ilemela.

"Fedha zote tunazozipokea zinakuja kwa maelekezo yake na sisi tunasimamia ili zifanye kazi husika ila hatukatazwi kuwa wabunifu katika kutengeneza njia mbadala wa kuondoa chanagamoto zilizoko katika wilaya yetu" - Hassan Masala, Mkuu wa wilaya Ilemela.

"Bado tuna changamoto mbalimbali katika wilaya yetu Ilemela. Tuna upungufu wa vyumba vya madarasa, tuna changamoto ya nyumba za walimu za kuishi ili kuendelea kuwapa Elimu watoto wetu, nazo tunaangalia njia ya kuzitekeleza" - Hassan Masala, Mkuu wa wilaya ya Ilemela.

"Kwa sababu pesa tulichangisha hadharani, tumeona pia tuwaite muone madawati tuliyoyatenga baada ya kuwashirikisha katika uchangiaji wa pesa za ununuzi wa madawati tuliofanya pamoja" - Hassan Masala, Mkuu wa wilaya Ilemela.

"Nakosa maneno mazuri ya kusema, ila ninaomba mpokee shukurani kutoka Serikalini, pokea shukurani zetu kutoka wilaya ya Ilemela na viongozi wake" - Hassan Masala, Mkuu wa wilaya Ilemela.

"Kama mkoa tumeanzisha opereseheni kabambe ya kuondoa upungufu wa madarasa, na Mkuu wa Mkoa wetu Robert Gabriel ameanza ziara katika wilaya zote kuona tunaziondoaje" Hassan Masala, Mkuu wa wilaya Ilemela.

"Taifa lote likipata Elimu, limepata maendeleo" - Mstahiki Meya Halmashauri Ilemela Renatus Mulunga.

"Ninawashukuru sana wadau wa maendeleo katika wilaya ya Ilemela, siku zote mmekuwa wabunifu wa kuanzisha miradi ya kuwasaidia wananchi. Nishukuru viongozi wote kwa kuwa bega kwa bega kuiendeleza Ilemela" - Dr Angeline Mabula, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Ilemela.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages