Breaking

Tuesday 26 July 2022

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA BALOZI




Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Caroline Kitana Chipeta kuwa Balozi wa Tanzania, The Hague nchini Uholanzi.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumanne Julai 26, 2022 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.

Balozi Chipeta alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages