Breaking

Thursday 21 July 2022

HAJI MANARA AFUNGIWA MIAKA MIWILI NA FAINI


Kamati ya Maadili ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) leo Alhamisi Julai 21, 2022 imetoa maamuzi kuhusiana na sekretarieti kufungua kesi katika kamati hiyo dhidi ya afisa habari wa Yanga Haji Manara.


Kamati ya maadili ya TFF imemkuta na hatia Haji Manara na kumfungia miaka miwili kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi na faini ya Tsh milioni 20 kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF Wallace Karia


Haji Manara alipishana kauli ya Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika eneo la VVIP wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages